Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Dkt. Nchimbi: Tumieni Vitambulisho Hivi Kuongeza Tija Katika Ujasiriamali
Dec 17, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_38952" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wajasiriamali wa mjini Singida waliopata mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) na Manispaa ya Singida ambapo katika hafla ya kufunga mafunzo hayo alitoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuwatambua na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao bila kubugudhiwa.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga mkoani Singida wameaswa kutumia vizuri fursa ya kupewa vitambulisho maalum vya kuwatambua ili waweze kuongeza tija katika shughuli zao.

Akizungumza wakati akiwakabidhi vitambuslisho hivyo mjini Singida , mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa Dhamira safi ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kuwezesha kundi hilo kufanya biashara bila kubugudhiwa ni ya kupongezwa na kuungwa mkono na kila mtanzania.

" Mhe. Rais Dkt. Magufuli anawapenda sana wajairiamali wadogo maarufu kama wamachinga ndio maana ameweka utaratibu huu mzuri wa kuwa na vitambulisho ambavyo haviuzwi na  kwa wale wenye sifa  za kupewa  mnachngia kiasi kidogo tu ambacho ni elfu 20,000 kwa mwaka"; Alisisitiza Dkt. Nchimbi.

[caption id="attachment_38953" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimvisha kitambulisho mmoja wa wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga wakati wa hafla iliyofanyika mjini Singida mwishoni mwa wiki ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.[/caption] [caption id="attachment_38954" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa na sehemu ya wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga mara baada yakuwapatia vitambulisho maalum vya kuwatambua vilivyolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya juhudi zake kuinua kundi hilo , hafla iliyofanyika mjini Singida mwishoni mwa wiki.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa wale wenye sifa za kupewa vitambulisho hivyo watapewa na wanao wajibu wakivitumia vizuri  ikiwa ni sehemu ya kutambua  mchango unaotolewa na Mhe. Rais wa Awamu ya Tano katika kuwainua kiuchumi na kijamii ili kuchochea ustawi wao na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa  kwa sasa kundi hilo lina fursa ya kushiriki kikamilifu katika kukuza biashara zao kutokana na mazingira yaliyowekwa na Serikali katika kuliwezesha kundi hilo ambapo wajasirimali hao sasa watapanua wigo wa kufanya shughuli zao bila kubugudhiwa.

Vitambulisho vinawawezesha kufanya biashara katika eneo lolote hapa nchini ilimradi wazingatie sheria kanuni na taratibu katika utekelezaji wa shughuli zao.

[caption id="attachment_38955" align="aligncenter" width="900"] Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Singida Bw. Apili Mbaruku akieleza umuhimu wa vitambulisho maalum vinavyotolewa kwa wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa tija. (Picha na MAELEZO- Singida)[/caption]

Kwa upande wake  Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Singida Bw. Apili Mbaruk amesema kuwa moja ya sifa ya kupewa kitambulisho hicho ni kuwa na mauzo yasiyozidi shilingi elfu 10,000/ kwa siku, Sifa nyingine ni kuwa na mauzo ghafi yasiyozidi milioni 4  kwa mwaka.

Akifafanua amesema kuwa ni kosa kisheria kwa mjasiriamali kutoa taarifa za uongo ili kupatiwa kitambulisho hicho hivyo ni vyema wale tu wenye sifa stahiki wakajitokeza na kuopatiwa vitambulisho hivyo.

Vitambulisho vilivyotolewa kwa kila mkoa hapa nchini ni elfu 25,000 vikilenga kuleta ustawi kwa wajasiriamali wadogo marufu kama wamachinga.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi