Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mamlaka za Maji Zaaswa Kutumia TEHAMA Kuimarisha Ukusanyaji Mapato
Nov 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37876" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akisisitiza umuhimu wa Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa Maji Mikoa kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa weledi ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa wanawafikisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.hayo yamejiri leo Jijini Dodoma wakati wa akifungua Kikao kazi cha siku mbili kwa watendaji hao leo Jijini Dodoma.[/caption]

Mamlaka za Maji Zaaswa Kutumia TEHAMA   Kuimarisha  Ukusanyaji  Mapato

Na: Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa amewataka Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa Maji kuhakikisha wanatumia  mifumo ya TEHAMA katika kukusanya mapato ili kuongeza ufanisi katika mamlaka hizo.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kinachowashirikisha Watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na Wahandisi wa maji wa mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma chenye lengo la kujenga uwezo kwa watendaji hao ili  kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha wananchi  wote wanafikiwa na huduma ya majisafi na salama.

[caption id="attachment_37877" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumzia umuhimu wa watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na wahandisi wa mikoa kusimamia miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kuzingatia uzalendo na uadilifu.[/caption] [caption id="attachment_37878" align="aligncenter" width="900"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa Mikoa, kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili.[/caption]

“Matumizi ya TEHAMA yatasaidia Mamlaka zote kuongeza mapato yake hali itakayosaidia kuimarisha huduma zinazotolewa kwa wananchi kwa kutumia fedha zitakazokusanywa na dhamira yetu kama Viongozi ni kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na huduma hii”; Alisisitiza Mhe. Prof. Mbarawa

Akifafanua amesema kuwa Baadhi ya Mamlaka zimeanza kutumia mifumo hiyo na imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuongeza mapato kutoka wastani wa Bilioni 8.2 hadi bilioni 10.1 kwa sasa yakiwa ni mafanikio ya kupigiwa mfano.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi  ya maji isiyoridhisha Prof. Mbarawa amesema Serikali haitatoa kazi kwa mkandarasi  ambaye ameshindwa kutekeleza mradi  aliopewa  ili iwe fundisho kwa wakandarasi wengine.

[caption id="attachment_37879" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa Mikoa yote hapa nchini.[/caption] [caption id="attachment_37880" align="aligncenter" width="898"] Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akiwa na watendaji wengine wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na wahandisi wa mikoa leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37881" align="aligncenter" width="886"] Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa Mikoa yote hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufungua kikao kazi hicho cha siku mbili.[/caption] [caption id="attachment_37882" align="aligncenter" width="772"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akizungumza wakati wa hafla ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa maji wa mikoa .[/caption] [caption id="attachment_37883" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya washiriki wa Kikao kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na Wahandisi wa maji wa mikoa kinachofanyika kuanzia leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37884" align="aligncenter" width="893"] Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na sehemu ya washiriki wa Kikao kazi cha siku mbili kinachowashirikisha watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na Wahandisi wa mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma.(Picha na Frank Mvungi- MAELEZO)[/caption]

Kuanzia sasa mkandarasi atakayeshindwa kutekeleza mradi wa maji katika eneo lolote hapa nchini asitarajie kupata kazi za miradi ya maji katika eneo lolote hapa nchini ili kuleta nidhamu kwa wale wanaopewa miradi.

Pia, Waziri Mbarawa ameagiza Mamlaka za Maji kutenga sehemu ya mapato yake kwa ajili ya kupanua huduma zake kwa wananchi.

Aidha, Waziri Mbarawa amebaisnisha kuwa Serikali imewekeza kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo katika Jiji la Dar es Salaam ambapo bilioni 800 zimewekezwa, Arusha bilioni 500 na mradi wa Shinyanga Tabora Nzega takribani bilioni 600.5 zinatumika katika utekelezaji wa mradi huo.

“Kwa upande wa watendaji wa Mamlaka za Maji na Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema kuwa mhandisi si kupata degree bali kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi yatakayosaidia wananchi kupata maji safi na Salama”; Alisisitiza Mhe. Prof. Mbarawa.

 Wizara ya Maji imekuwa ikichukua hatua za makusudi katika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wote, Kikao Kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na Wahandisi wa mikoa ili kujenga uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi