Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watu 6000 Jimboni Kwa Waziri Lukuvi Wanufaika na Msaada wa Maji Toka Agakhan
Sep 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

 

Waziri  wa ardhi  nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam  Lukuvi  ambae ni  mbunge  wa   jimbo la  Ismani  (kushoto ) akishirikiana na  makamu Rais wa  jumuiya ya  Ismailia nchini  Tanzania Kamal Khimji (kulia) wakisaidiana kuwatwisha ndoo  za  maji wanawake  wakazi wa Mapogolo jimbo la Isimani wilayani Iringa wakati wa  uzinduzi wa visima  viwili  vya maji ya  kutumia umeme  wa  jua (solla Power)  vilivyochimbwa kwa ufadhili wa madhehebu ya ya  Shia Imami Ismailia ya Tanzania  kupitia  taasisi  ya kusini kwa  kushirikiana na Agakhan  Development Network (ADKN) juzi kwenye  vijijivya Mapogolo na  Ikorongo
Waziri  Lukuvi na  viongozi  mbali mbali  wakitazama  nguma ya  njuga   ikichezwa na  watoto wa  shule ya msingi  Idodi
Waziri  Lukuvi  akimhoji  mmoja katika ya  wasanii wa ngoma ya njuga
Makamu wa Rais  wa  Ismailia  nchini Tanzania Kamal Khimji akisalimiana na viongozi  mbali mbali  baada ya kuwasilia katika  sherehe ya  uzinduzi wa  visima
Makamu  wa  Rais  wa  Ismailia  nchini  Tanzania Kamal Khimji akieleza  jambo
Waziri  Lukuvi  akisalimiana na makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza akisalimiana na makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji baada ya  kuwasili kijiji  cha Mapogolo  jimbo la  Ismani
 makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji akitoa  hotuba  yake
Viongozi  mbali  mbali  wa  Ismailia  na  viongozi wa  serikali  wakisikiliza  hotuba ya  makamu wa  Rais wa  jumuiya ya  Ismailia  nchini
Umati wa  wananchi   walioshiriki  sherehe ya  uzinduzi  wa visima  viwili  vilivyotolewa  msaada  na   Agakhan  Iringa
Viongozi  wakifuatilia  uzinduzi  wa  visima  vilivyotolewa msaada  na Agakhan
Fundi  wa  visima  hivyo  akitoa  maelekezo  kwa  viongozi  mbali mbali
Waziri  Lukuvi  (kushoto)  na makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji wakizindua  moja kati ya  kisima katika kijiji cha Mapogolo
 makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji (kushoto) na  waziri Lukuvi wakizindua  kisima
makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji akitoa  maelekezo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  baada ya kuzindua  kisima
Waziri  Lukuvi  akimpongeza  na makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji
Bango la  kisima  cha Ikorongo  likizinduliwa katika hafla hiyo
Waziri  Lukuvi  na makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji na  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  wakisikiliza kwa makini wakati DC  Iringa  Richard Kasesela  akisoma jiwe  la  msingi  baada ya  uzinduzi wa visima
Waziri  Lukuvi  kushoto  wakishirikiana na  makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji kufungua  maji  ya  bomba  baada ya  kuzinduliwa  kwa visima  viwili  chini ya ufadhili wa Agakhan  visima  vitakavyonufaisha  watu 6000 wa vijiji  vya Mapogolo kata ya Idodi na Ikorongo kata ya Itunundu  jimbo la Ismani
 makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji akimtwisha  ndoo ya maji mwanamke mkazi wa Mapogolo  baada ya  kuzindua  visima  viwili
Lukuvi  akimtwisha maji  mkazi wa Mapogolo
 makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji akivishwa  mgolole  nguo  za  heshima ya  kichifu kabila la  wahehe  kama  heshima kubwa ya  kusaidia  jamii
 makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji akiwa katika  vazi la  kichifu  na  viongozi  mbali mbali baada ya  kuzawadiwa kama  ahsante  kwa Agakhan  kusaidia  jamii
Viongozi wa chama  tawala  na  serikali wakiwa katika picha ya pamoja na  makamu  wa  Rais  wa  Jumuiya ya  Ismailia nchini Kamal Khimji (picha na habari  na MatukiodaimaBlog)
TAKRIBANI watu 6000 katika  jimbo la  Ismani wilaya ya  Iringa  mkoani  Iringa wafaidika na mradi  wa maji ya visima  vinavyotumia umeme  wa  jua  (solla Power) kutoka Agakhan.
Akizungumza jana katika  kijiji  cha Mapogolo kata ya  Idodi  wakati wa  sherehe  ya  uzinduzi  wa  visima  hivyo viwili mbunge  wa  jimbo la  Ismani Wiliam Lukuvi  ambae ni  waziri  wa ardhi  nyumba na maendeleo  ya makazi aliwashukuru  wafadhili wa  visima   hivyo  kutoka  madhehebu ya  Ismailia pamoja na taasisi yao  kutoka kusini iliyoshirikiana na  taasisi ya Agakhan Development Network (ADKN)  kuwa  amefurahishwa na  jitihada  hizo.
" Nimefurahishwa na  kuona jumuiya  ya Ismailia  kupitia taasisi yao kutoka kusini  kwa  kushirikiana  na Agakhan Development Network (AKDN) walioona umuhimu  wa upatikanaji wa  maji kupitia umeme  wa  jua na kupendekeza hiyo  miradi kwenye miradi yao  mbali mbali inayoendelea na  miradi  mingine hapa  nchini kwenye mwaka huu wanaosherekea maadhimisho  ya  miaka  60 ya  mtukufu Agakhan tangu awe imamu wa  madhehebu  ya jumuiya ya Ismailia"
Alisema  kuwa  Agakhan  Development (AKDN) ni  taasisi iliyoundwa na mtukufu  Agakhan  kwa  zaidi ya  miaka mia moja imeendelea kukuza na  kuboresha maendeleo  ya nchi ya  Tanzania  kwa kuwekeza kwenye sekta  ya elimu ,kilimo na kuboresha  miundo mbinu  ili kukuza uchumi na maisha  bora kwa  watanzania .
Katika  sherehe  hiyo ya  uzinduzi  wa  visima  viwili  vitakavyohudumia  wananchi  wa  vijiji  vya  Mapogolo, na Ikorongo pia  ilihudhuliwa na makamu  wa  Rais  wa jumuiya ya Ismailia nchini Tanzania Kamal Khimji alipata  kuhudhuria  pamoja na  viongozi mbali  mbali  wa  mkoa  wa  Iringa wakiongozwa na mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza .
>

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi