Makampuni kumi na tano (15) yaliojumuisha wazalishaji pamoja na wasafirishaji wa bidhaa za Mbogamboga na Matunda wajiongezea fursa katika soko la Ulaya kufuatia Ushiriki wao katika Maonesho ya Kimataifa ya Mbogamboga na Matunda yajulikanayo kama Fruit Logistica 2020 yaliyofanyika tarehe 5 hadi 7 Februari, 2020 mjini Berlin nchini Ujerumani.
Mazao yaliyovutia wanunuzi na wadau wengine katika maonyesho hayo ni pamoja na parachichi, rasiberi, pasheni, ndimu zisizo na mbegu, njegere, snow peas na sugar snaps, maharage machanga (green beans), fre...
Read More