Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Jenerali Mabeyo Azindua Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma
Feb 26, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51239" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akikata utepe kuzindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Februari 26, 2020.[/caption]

Na Frank Mvungi

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amezindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Akizungumza leo Februari 26, 2020 wakati akizundua makao makuu hayo Jenerali Mabeyo amesema kuwa, JKT imekuwa yakupigiwa mfano kwa utendaji unaotokana na utekelezaji mzuri wa miradi yote waliyokabidhiwa.

[caption id="attachment_51240" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbunge baada ya kuzindua Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.[/caption]

“Nawapongeza JKT kwa kutekeleza kikamilifu miradi ya ujenzi wa ukuta wa Mirerani, Ujenzi wa ukuta wa Ikulu ya Chamwino, Ujenzi wa ukuta wa uwanja wa ndege Ngerengere,Ukamilishaji wa nyumba za Jeshi la Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam na miradi yote mliyokabidhiwa mlitekeleza kwa wakati, ubora na viwango hali iliyowajengea heshima “, Alisisitiza Jenerali Mabeyo

Akifafanua Jenerali Mabeyo amesema kuwa ni wakati muafaka kwa JKT kujipanga kwa kujiimarisha kwa kununua mitambo na vifaa zaidi ili kujenga uwezo wa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa pasipo kutegemea vifaa na nyenzo za kukodi au kuazima.

[caption id="attachment_51241" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.[/caption]

Aliongeza kuwa ili kuendelea kujenga heshima ya JKT kwa Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli ni vyema utekelezaji wa miradi yote ukaendelea kuwa katika ubora unaotakiwa, uzingatiaji wa Sheria ya manunuzi na taratibu zote zilizowekwa na Serikali.

Aidha, Jenerali Mabeyo amewaasa Maafisa na Watumishi wa Umma watakaotumia majengo ya makao makuu hayo kuyatunza ili yaweze kudumu kwa kuwa ujenzi wake umetumia rasilimali nyingi.

[caption id="attachment_51242" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akipanda mti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Februari 26, 2020.[/caption]

Katika hatua nyingine Jenerali Mabeyo amesema kuwa JKT inapaswa kujipanga kwa kuwa itahusika katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Ulizi wa Taifa katika Wilaya hiyo.

Uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT umefanyika Bwigiri Wilayani Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Wakuu wa Jeshi hilo wastaafu, Maafisa wa ngazi mbalimbali,ss Watumishi wa Umma, Wananchi na viongozi wa Wilaya hiyo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi