Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Nchi za SADC Kuweka Sheria ya Kusimamia Miradi ya Kimkakati ya Sekta ya Nishati
Feb 28, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51264" align="aligncenter" width="750"] Kamishina wa Mafuta na Gesi kutoka Wazira ya Nishati, Bw.Adam Zuberi akiendesha Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika Leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.[/caption] [caption id="attachment_51265" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Miundombinu Sekritarieti ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Mapolao Rosemary Makoena akiwa kwenye Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka nchi wanachama ulimalizika leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Wataalamu wa Nishati katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imependekeza mataifa hayo kuwa na sheria rasmi za kusimamia miradi ya kimkakati katika sekta ya nishati ili kuwa na utoshelevu wa uhakika wa nishati ya umeme kwa ajili mahitaji ya wananchi wake. Hayo yamesemwa leo Ijumaa (Februari 28,2020) Jijini Dar es Salaama na Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati,Adam Zuberi wakati akifunga mkutano wa siku nne wa Kamati ya Wataalamu wa Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichoanza tarehe 24-28 Februari mwaka huu.Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania

[caption id="attachment_51267" align="aligncenter" width="750"] Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia mkutano huo uliomalizika leo leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.[/caption]

Alisema katika kikao hicho, wajumbe hao walitoa mapendekezo mbalimbali yanayotarajiwa kujadiliwa kwa pamoja katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo kinachotarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu, ambapo moja ya mapendekezo yaliyokubaliwa na wataalamu hao ni pamoja na kuweka sheria rasmi ya kusimamia  taasisi za kimkakati katika sekta ya nishati ndani ya SADC.

‘’Katika SADC tuna miradi mikubwa ya kimkakati ambayo sasa tumekubaliana iende mbele zaidi kwa Mawaziri ikiwemo kusaini MOU (mkataba wa makubaliano) ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo inaweza kufanya kazi’’ alisema Zuberi.

Aliongeza kuwa miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotarajiwa kupewa kipaumbele katika uendelezaji wake ni pamoja na Uimarishaji wa Kituo cha Umahiri katika Uendelezaji wa Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya  Nishati (SACREEE) pamoja  na kuratibu utoaji wa mafunzo kwa wataalamu kuhusu nishati ya umeme.

[caption id="attachment_51269" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi kutoka Msumbiji akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.[/caption]

Alibainisha mradi mwingine ni pamoja na uendelezaji wa kituo cha umahiri cha kafue uliopo nchini Zambia, ambacho kitatumika kama chombo rasmi cha Jumuiya hiyo kitakachotumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya nishati katika jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa Zuberi alisema mapendekezo mengine yaliyojadiliwa kwa mapana na wataalamu hao SADC ni makubaliano ya pamoja katika kuwa na miradi ya pamoja ya kimkakati kuunganisha nchi moja na nyingine ili kuhakikisha kuwa nchi za SADC zinakuwa na nishati ya umeme wa uhakika.

[caption id="attachment_51270" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi kutoka Tanzania akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.[/caption]

Kwa mujibu wa Zuberi alisema mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja na kuwa na mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia (2012-2027)ambapo kwa sasa tayari mshauri mwelekezi tayari amepatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo mwezi Agosti mwaka jana.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundmbinu wa SADC Bi. Rosemary Makoena alisema katika kikao hicho wataalamu hao walijikita katika kujadili namna bora ya kusimamia matumizi ya nishati mbadala ili kuweka kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kwa kutosheleza kiwango cha mahitaji ya nishati ya umeme katika SADC.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi