Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yapongezwa Kwa Hatua za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia
Feb 28, 2020
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_51254" align="aligncenter" width="750"] Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati akifungua Kongamano la Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dodoma Februari 27, 2020.[/caption]

Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini.

Akizungumza wakati akifungua  Kongamano la   Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani   Jijini Dodoma Februari 27, 2020, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda amesema kuwa Serikali imechukua hatua zilizosaidia kupunguza vitendo hivyo.

“ Serikali imechukua hatua za makusudi kutoa elimu bure, mikopo kwa akina mama, vijana na walemavu ili kuleta ustawi wa wananchi na kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia”,Alisisitiza Mhe. Makinda

[caption id="attachment_51255" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupunguza na kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa Nchini, hayo yamejiri Februari 27, 2020.[/caption]

Akifafanua amesema Serikali inachukua hatua zinazolenga kuleta tija kwa wananchi ikiwemo kufikisha huduma za umeme Vijijini, kuboresha huduma za afya kupitia ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za Wilaya na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani zinafanyika shughuli mbalimbali ikiwemo misafara, makongamano na midahalo.

Aliongeza kuwa Serikali imekuwa ikichukua hatua katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zikiwemo zinazosimamia sheria.

[caption id="attachment_51256" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Taifa linaloshughulikia Wanawake (UN Women) Bi. Hodan Addou akizungumza katika Kongamano hilo ambapo alipongeza juhudi za Serikali katika kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia[/caption] Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake Bi. Hodan Addou ameipongeza Serikali kwa hatua inazochukua katika kuhakikisha inakomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia. Aliongeza kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia program zinazosukuma mbele ajenda za usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake. Kongamano la   Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani limefanyika   Jijini Dodoma Februari 27, 2020 ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani. [caption id="attachment_51257" align="aligncenter" width="750"] Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kongamano la Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dodoma Februari 27, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51258" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (wenye sare) wakifuatilia Kongamano la Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dodoma Februari 27, 2020 kutoka Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_51259" align="aligncenter" width="750"] Washiriki wa Kongamano la Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika Jijini Dodoma Februari 27, 2020 wakifuatilia hotuba ya Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo.[/caption]

(Picha zote na Frank Mvungi)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi