Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga mradi wa kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya mto Rufiji, Stiegler’s Gorge utasaidia sana kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.
Akizungumza baada ya kutembelea eneo utakapojengwa mradi huo, leo (Alhamisi, Oktoba 4, 2018), Waziri Mkuu amesema umeme utakaotokana na maji, utazalishwa kwa gharama nafuu na utakuwa wa uhakika zaidi.
Amesema kwa vile umeme utakaozalishwa katika mradi wa Stiegler’s Gorge utakuwa wa bei nafuu na hivyo kuwa rafiki kwa wananchi wa kipa...
Read More