Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (katikati), akiongoza kikao cha majadiliano kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania kuhusu masuala kadhaa ikiwemo maombi ya Tanzania kwa benki hiyo, kufadhili Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na ukarabati wa Reli ya Kati (MGR), ambapo Benki hiyo imekubali kutoa fedha baada ya kukamilika kwa taratibu za ndani za pande hizo mbili. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, Kulia kwake ni Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohammed Mchengerwa, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayesimamia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila na kushoto kwake ni Mkurugenzi mkazi wa Benki hiyo, Bw. Nathan Belete na ujumbe kutoka Benki hiyo.
Read More