Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Picha: Ziara ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI JKCI
Feb 22, 2024
Picha:  Ziara ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Afya na UKIMWI JKCI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Mhe. Waziri ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni na kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt.Godwin Mollel.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni akizungumza na vyombo vya habari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

 

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Deogratis Nkya akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI  jinsi wanavyofanya upasuaji wa kuzibua tundu la moyo wa mtoto bila ya kufungua kifua wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Dkt. Nkya, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni .

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi