Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesamehe jumla ya wafungwa 8,157 katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri, Mjini Dodoma.
Msamaha huo umehusisha wafungwa 1828 ambao watatolewa kaunzia leo na wengine 6329 wamepunguziwa muda wa vifungo vyao, aidha kati ya wafungwa watakaoachiwa huru wafungwa 61 ni wafungwa ambao walihukumiwa kunyongwa.
“Kuna wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa wana umri wa miaka 85 na wapo waliokaa gerezani zaidi miaka...
Read More