Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea shamba la ufugaji wa ng'ombe wa maziwa la Alesandra lilipo Milan nchini Italia, ambalo linaendeshwa kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kielektoniki ikiwemo ukamuaji wa maziwa kwa kutumia roboti. Akiwa katika shamba lenye takribani ngo'mbe 500, Mheshimiwa Majaliwa ameshuhudia mifumo bora ya ufugaji, ulishaji , unyonyeshaji na ukamuaji wa maziwa, ambapo ng'ombe mmoja ana uwezo wa kutoa lita kuanzia 35 hadi 70 kwa siku na kumuwezesha Mfugaji kupata tija zaidi. Waziri Mkuu alitembelea shamba hilo...
Read More