Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Atembelea Maeneo Yaliyoathirika na Mafuriko Katesh, Atembelea Wagonjwa
Dec 07, 2023
Rais Samia Atembelea Maeneo Yaliyoathirika na Mafuriko Katesh, Atembelea Wagonjwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom ambalo limeathirika na mafuriko pamoja na maporomoko ya matope na mawe wilayani Hanang' mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ndugu Elibariki Naman mkazi wa Jorodom, Katesh ambaye ni muathirika wa mafuriko yaliyotokea wilayani Hanang. Ndugu Elibariki alikuwa akielezea jinsi majirani zake walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao katika maafa hayo 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga akielezea kuhusiana na athari za mafuriko yaliyotokea katika eneo la Jorodom Katesh wilayani Hanang. Rais Samia ametembelea eneo hilo mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Bi. Christina Nyangole pamoja na mtoto wake Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Bi. Christina na Mtoto wake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh, Hanang mkoani Manyara.

 

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi