Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa ametembelea mabanda ya Wajasiriamali wanaoshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea kufanyika Bujumbura, Burundi.
Akiwa katika maonesho hayo, Balozi Byakanwa amewataka wajasiriamali kuendelea kufanya biashara zao kwa tija na ufanisi, pia amewahimiza kutumia fursa hiyo kutafuta masoko zaidi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Vili vile, ameipongeza Serikali kwa kuwezesha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania kushiriki maonesho ambayo yanasaidia kukuza ajira na kupanua masoko ya bidhaa na huduma zao.