Na mwandishi wetu
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2020 umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi Ruth Minja amesema kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia ,mwezi Desemba, 2019....
Read More