Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Julai, 2020 amewaapisha Wakuu wa Mikoa 2, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya 1 na Katibu Tawala wa Mkoa 1, na pia ameshuhudia Wakuu wa Mikoa wakiwaapisha Wakuu wa Wilaya 9 Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Kamishna wa Polisi Thobias Emir Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Philemon Rugumiliza Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa Tabora, Bw. James Wilbert Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka...
Read More