Na Lulu Mussa, Songwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. MussaSima ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Songwe kuwabaini, kuwasajili nakuunda vikundi vya wachimbaji wadogo wasio rasmi ili waweze kutambulikana kufaidika na mikopo midogo midogo inayotolewa na Serikali hapa nchini.
Ameyasema hayo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Mkoawa Songwe hususan Wilaya ya Songwe na kubaini changamoto ya wachimbaji wadogo wanaoharibu mazingira kutokana na uchimbaji holela.
“Ni lazima mchukue hatua za haraka za kuwatambua wachimbaji hawa kwalengo la kuwasajili na kuanzisha kanzi data itakayosaidia katika zoezi lautoaji wa elimu ili kunusuru mazingira” Sima alisisitiza.Waziri Sima
Amesisitiza kuwa ni vema pia Wilaya ya Songwe ikaanzisha vikundi vya mazingira na kuhamasisha matumizi ya Sheria ndogondogo katika maeneo yao.
Akiwasilisha taarifa ya hali ya Mazingira katika Wilaya hiyo Mkuu wa Wilayaya Samuel Jeremia Opulukwa amesema Wilaya yake inakabiliwa nachangamoto kubwa za uchomaji wa misitu unaohatarisha maisha ya viumbehai na ikolojia ya eneo hilo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka ametoa wito kwa watafiti wa madini katika eneo hilo kutoa taarifa rasmi katika ngazi ya Wilaya ili kuepuka uharibifu wa mazingira unaofanywa na watafiti hao kwakuchimba kiholela kwa lengo la kutafuta dhahabu.
Pia, Naibu Waziri Sima ametembelea Mgodi wa Shanta na kuagiza uongozi wa mgodi huo kutoa elimu kwa jamii inayozunguka mgodi huo juu ya namna bora ya uchimbaji wa madini kwa njia bora na salama kwa mazingira.
“Kwa kuwa mgodi huu unatumia teknolojia ya kisasa zaidi, natoa rai kwamgodi kuhamisha teknolojia hii kwa wachimbaji wadogo wadogo ili wananchipia wanufaike” Sima alisisitiza.
Mheshimiwa Mussa Sima yuko Mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi naametembelea Wilaya ya Songwe na kukagua usimamizi na uzingatiaji waSheria ya Mazingira ambapo kesho atawasili Mkoani Mbeya