TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 25 Septemba, 2021 amerejea Jijini Dar es Salaam akitokea New York nchini Marekani alipokuwa akihudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Rais Samia amepokelewa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla, viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa, viongozi wa dini pamoja...
Read More