Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amevaa Kifaa Maalum cha kumuwezesha kuona kwa ukaribu matukio mbalimbali duniani kijulikanacho kama Teknolojia Ukweli Halisi (Virtual Reality Device) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh wakishuhudia tukio hilo.
Read More