Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

COSTECH Kupaisha Sayansi na Teknolojia
Aug 25, 2023
COSTECH Kupaisha Sayansi na Teknolojia
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Agosti 24, 2023.
Na Na Mwandishi Wetu

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuendelea kusimamia miradi ya Kigoda cha Utafiti inayoendelea katika chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM-AIST) Arusha.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt. Amos Nungu leo agost 25, 2023 jijini Dodoma wakati akieleza utrekelezaji wa majukumu ya Tume  hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa maka wa fedha 2023/2024.

“Uanzishwaji wa Vigoda viwili vya utafiti  katika chuo Kikuu SUA na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM-AIST) Arusha vina thamani ya Dola za Kimarekani milioni 2 ambazo ni  takribani Shilingi bilioni mbili na nusu za kitanzania kwa kila kigoda kimoja, huu ni mradi wa miaka mitano na kwa sasa tupo mwaka wa pili, wasimamizi wa Vigoda ni wabobezi wa utafiti katika maeneo yao, vinatumika kuleta mhusiano zaidi na watafiti wengine, pia fursa ya mafunzo kwa vijana wetu” amefafanua Dkt. Nungu.

Aidha, amebainisha kuwa kwa mwaka huu Tume hiyo itaendelea kushirikiana na Mabaraza ya Kikanda na Kimataifa ili kuhakikisha wanatafuta fursa ambazo zitaendelea kuleta fedha za utafiti kupitia COSTECH au kuhamasisha Taasisi za ndani kuomba hizo fursa.

Mbali na hayo, Dkt. Nungu amesema kuwa, katika kuratibu Utafiti na Ubunifu, COSTECH itaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali kwa lengo la  kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha, sera na miongozo stahiki, mashirikiano, miundombinu, na kuhakikisha mchango wa utafiti na ubunifu unaleta manufaa kwa taifa.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), iliundwa kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Na. 7 ya Bunge ya mwaka 1986 na kuzinduliwa tarehe 30 Juni 1988. Ni taasisi ya Muungano iliyorithi majukumu ya lililokuwa Baraza la Taifa la Utafiti (Tanzania Scientific Research Council) kwa kifupi ‘UTAFITI’. Baraza la Taifa la Utafiti liliundwa kwa mujibu wa Sheria Na. 51 ya Bunge ya mwaka 1968 na kuzinduliwa rasmi tarehe 25 Juni 1972.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi