[caption id="attachment_33591" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Ukune katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018.[/caption] [caption id="attachment_33592" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba. (kushoto) wakati alipokagua uuzaji wa tumbaku katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu, Julai 16, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Nchini, Dkt. Titus Kamani.[/caption] [caption id="attachment_33593" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kangeme kwenye Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018.[/caption] [caption id="attachment_33594" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari alilolizindua ambalo limenunuliwa na Halmashauri ya Ushetu kwa ajili ya Idara ya Kilimo ya Halmashauri hiyo kwenye kijiji cha Kangeme Julai 16, 2018.[/caption] [caption id="attachment_33595" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Fao la Ushirika Afya ambalo litawawezesha wanaushirika kunufaika na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwenye kijiji cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga Julai 16, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, watatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption]