Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ziara ya Naibu Waziri Maliasili na Utalii katika Shamba la Miti Sao Hill na Kituo cha Malikale cha Ismila na Kalenga Mkoani Iringa
Oct 31, 2017
Na Msemaji Mkuu

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipotembelea shamba la miti Sao Hill kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika shambani hapo. Aliagiza uongozi wa shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akikagua baadhi ya vifungashio vya asali alipotembelea shamba la miti Sao Hill kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika shambani hapo. Asali inayozalishwa na shamba hilo imefanyiwa vipimo nchini Ujerumani na kugundulika kuwa ni bidhaa bora isiyo na viambata vya kemikali ya aina yeyote. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na Afisa Ufugaji Nyuki wa shamba hilo, Said Abubakar. 
Meneja wa shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko (kushoto) akimueleza Mhe. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) kuhusu moto uliovamia hekta 77 za shamba hilo na hatua zilizochukuliwa kuudhibiti alipotembelea kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika shambani hapo, alisema moto huo uliozuka hivi karibuni ulianzia kwenye mashamba ya wananchi haukuwa na madhara makubwa. 
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga kuhusu utafiti unaofanywa na shamba hilo kwa kushirikiana na Kampuni ya Art International kuhusu uvunaji wa utomvu kwa ajili ya kutengeneza madawa mbalimbali, bazooka (chewing gums) na ‘gel’ kwa ajili ya kujiongezea kipato alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika shambani hapo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mhe. Jamhuri David.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Laurent Nampunju (kulia) kuhusu fuvu la Chifu Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya chifu huyo kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo cha Mambo ya Kale cha Kalenga mkoani Iringa hivi karibuni. 
Jengo la Makumbusho ya Mkwawa ambalo lipo ndani ya Kituo cha Mambo ya Kale cha Kalenga Mkoani Iringa.
 Picha ya Chifu Mkwawa ambayo inapatikana katika makumbusho hayo.
Muonekano wa fuvu la Chifu Mkwawa ambalo pia linapatikana katika makumbusho hayo. (Picha na Hamza Temba - WMU)
      >

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi