Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Makonda Atoa Taswira ya AFCON 2027, Tanzania Yajipanga Kujitangaza Kimataifa
Jun 02, 2026
Waziri Makonda Atoa Taswira ya AFCON 2027, Tanzania  Yajipanga Kujitangaza Kimataifa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, akizungumza na hamasa wakati wa chakula cha pamoja na mashabiki wa timu hiyo kilichoandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa pamoja na Morocco Mhe. Balozi Said Yakubu.
Na George Lugeiyamu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yanaendelea vizuri, huku Serikali ikiendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu na huduma muhimu zitakazowezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa kiwango cha kimataifa.

Mhe. Makonda amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika yanafanyika kwa mafanikio makubwa, kupitia maboresho ya viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, huduma za usafiri, mawasiliano na malazi kwa maelfu ya wageni na timu zitakazoshiriki mashindano hayo.

Ameeleza kuwa maandalizi hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa karibu kati ya wizara mbalimbali, taasisi za Serikali na wadau wa sekta binafsi, kwa lengo la kuhakikisha viwango na masharti yote yaliyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yanazingatiwa katika kila hatua ya utekelezaji.

“Serikali inaendelea kufanya maandalizi kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa AFCON 2027 na kuonyesha uwezo wake wa kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa,” amesema Makonda. 

Aidha, amebainisha kuwa AFCON 2027 ni fursa adhimu kwa Tanzania kujitangaza katika jukwaa la kimataifa, kuvutia uwekezaji mpya na kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea  Tanzania wakati wa mashindano hayo huku sekta mbalimbali  zikiwemo biashara, utalii, usafirishaji, huduma za malazi na ajira zikitarajiwa kunufaika jambo litakalochochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Waziri Makonda ameendelea kuwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya mashindano hayo kwa kutoa ushirikiano unaohitajika na kutumia fursa za kiuchumi zitakazotokana na ujio wa AFCON 2027.

“Lengo letu ni kuona AFCON 2027 inaacha alama ya kipekee nchini, si tu katika maendeleo ya michezo, bali pia katika uchumi, utalii na taswira ya Tanzania duniani,” amesema.

Amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha AFCON 2027 inakuwa miongoni mwa mashindano yaliyofanikiwa zaidi katika historia ya soka la Afrika na kuacha urithi wa kudumu kwa vizazi vijavyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor