Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ziara ya Majaliwa Wilayani Lushoto
Oct 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37630" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga Oktoba 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge.[/caption] [caption id="attachment_37631" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge wakati alipotembelea ofisi mpya za Halmshauri hiyo baada ya kuzindua jengo la utawala, Oktoba 31, 2018.[/caption] [caption id="attachment_37632" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la mbogamboga na matunda linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Malindi wilayani Lushoto, Oktoba 31, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.[/caption] [caption id="attachment_37633" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018.[/caption] [caption id="attachment_37634" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lukozi katika Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi