Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bwana Omari Khamis
Othman akizungumza na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kulia)
na Ujumbe aliofuatana nao alipomtembelea ofisini kwake, wakati akiendelea na
ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. Mkuu huyo wa Mkoa
aliahidi kushughulikia kwa karibu ombi lilitolewa na Kamishna Sururu la
kupatiwa viwanja kwenye maeneo yaliyotengwa na Serikali ili kujenga nyumba za
makazi ya askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoani humo.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
akisikiliza maelezo yanayotolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Iddi A. Iddi
wa Kituo cha Uhamiaji Bandari ya Wete kuhusu ukaguzi wa watu wanaotumia
Bandari hiyo ambapo vyombo vyake havijaruhusiwa kisheria kusafirisha abiria.
Ilielezwa kuwa hiyo ni changamoto kubwa katika Bandari hiyo kwani abiria wengi
wanaotumia Bandari hiyo hudai kuwa wanakwenda kwenye visiwa vya jirani vya
Fundo, Uvinje na Kokota, badala yake wakifika Bandari bubu zilizoko kijiji cha
Mtambwe wanabadili chombo kuelekea Visiwa vya Mombasa, Kenya. Yalisemwa hayo
wakati wa ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.
Mkuu wa Bandari ya Wete, Bwana Hassan Hamad Ali
akimpokea kwa ajili ya kukagua maeneo mbali mbali ya Bandari hiyo Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari M. Sururu (wa pili kushoto) na Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji
alioambatana nao katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21
Disemba, 2017. Kamishna Sururu alimtaka Mkuu huyo kushughulikia kwa karibu
changamoto iliyopo ya baadhi ya vyombo vya Usafiri “Majahazi” bandarini hapo
kupakia abiria kinyume cha Sheria.
Mkaguzi wa Uhamiaji, Omari Saidi Mohamed akimuonesha
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (katikati) na Maafisa
Waandamizi wa Uhamiaji aliombatana nao nyumba za makazi ya Askari wa Uhamiaji
zilizoko mtaa wa Mtemani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa
ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kutokana na uchakavu
wa nyumba hizo, Kamishna Sururu aliagiza nyumba hizo zifanyiwe ukarabati haraka
iwezekanavyo, huku akiahidi kwamba, Idara yake kwa kushirikiana na Serikali
Sheha wa Shehia ya Gando, Bw. Jafari Suleiman Said (wa
pili kulia) akizungumzia uwepo wa Bandari bubu ya Chokaani, Shehia ya Gando
Wilaya ya Wete inayotumiwa na baadhi ya watu kuingia na kutoka visiwani humo
kwenda visiwa vya Mombasa, Kenya. Hayo yalielezwa kwa Kamishna wa Uhamiaji
Zanzibar, Johari M. Sururu wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoa wa
Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa
pili kulia) akiwa mbele ya Jengo la Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Micheweni, Mkoa
wa Kaskazini Pemba iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na kujengwa uzio hivi
karibuni, akifafanua jambo kuhusu mkakati wa Idara wa kuboresha majengo ya
Ofisi na Makazi ya Askari wa Uhamiaji kwa Mikoa yote Unguja na Pemba. Huo ni
muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2018.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (wa
pili kushoto) akipokea salamu za Wananchi wa Shumba Mjini, akiwa katika ziara
ya kikazi tarehe 20 Disemba 2017, akitembelea Bandari Bubu iliyopo Shumba
Mjini, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambayo ni maarufu kwa
shughuli za Uvuvi na Biashara.
Mkuu wa Diko “Bandari Bubu” ya Shumba mjini
Bwana Hussein Rashid Omar, akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M.
Sururu wakati alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini
Pemba tarehe 20 Disemba, 2017, baadhi ya Majahazi (hayapo pichani) yanayofanya
safari zake kupitia Bandari bubu hiyo. Huku wananchi waliowazunguka
wakisisitiza kuwa wao wanuafata Sheria na Taratibu zote za Nchi wanapotoka ama
kuingia nchini ikiwemo matumizi ya Pasipoti na kuiomba Idara ya Uhamiaji
kusukuma mbele juhudi za Serikali kurasimisha Bandari hiyo
Sheha wa Shehia ya Kiuyu Mbuyuni, Bw. Ali Hamad
Sharifu (wa pili kulia) akimueleza Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M.
Sururu (kushoto kwake), jinsi wanavyoshirikiana na watendaji wa Idara ya
Uhamiaji kwa kutoa taarifa zinazosaidia kuwadhibiti baadhi ya Watu wasio
waaminifu wanaojaribu kuingiza wageni bila ya kufuata Sheria na Taratibu za
Idara ya Uhamiaji Nchini. Yalielezwa hayo wakati Kamishna akiendelea na ziara
ya kikazi, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 20 – 21 Disemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu
akiambatana na Maofisa waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar kukagua baadhi
ya bandari Bubu za Kiuyu na Mbuyuni, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini
Pemba wakati alipofanya ziara ya kikazi maeneo mbali mbali, Mkoani humo tarehe
20 – 21 Disemba, 2017. Wilaya ya Micheweni ina Bandari Bubu zaidi ya 80
Zinazotumiwa kuvuka mpaka wa majini kuingia Visiwa vya jirani pamoja na
Shimoni, Mombasa, Kenya ambapo wakaazi wa maeneo hayo wana muingiliano mkubwa
katika shughuli za kiuchumi na kijamii.