#Katika Mwaka wa Fedha 2018/19 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imetenga shilingi milioni 170 za kuifanyia matengenezo kwa urefu wa Km 8.5 barabara ya Mpunguzi - Ilangali - Mhe. Kadege.
#Kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 Serikali imetenga shilingi milioni 137.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Kiselya na Mlahango - Mhe. Kakunda.
#Serikali imeendelea na ujenzi wa shule mpya karibu na Shule ya Msingi Majimatitu ili kupunguza wingi wa wanafunzi waliopo katika shule ya Majimatitu - Mhe. Jafo.
#Hadi Julai, 2018 Benki ya Maendeleo ya Kilimo imeshatoa mikopo ya shilingi bilioni 48.67 iliyowanufaisha wakulima 527,291 - Mhe. Dkt. Mwanjelwa.
#Mradi wa kujenga uwezo wa kitaasisi ili kupanua mafunzo ya kiufundi katika sekta ya ufugaji samaki umeshaanza katika Bajeti ya mwaka huu - Mhe. Ulega.
#Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mpango wa kuboresha shamba la mifugo la Kitulo kwa kuboresha kosaafu za ng'ombe kwa kununua ng'ombe bora wa maziwa kutoka 450 waliokuwepo hadi kufikia 1200 ifikapo mwaka 2023 - Mhe. Ulega.
#Kwa mwaka wa Fedha 2018/19, jumla ya shilingi milioni 1,822.550 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Bigwa - Kisaki yenye urefu wa Km 133.28 - Mhe. Kwandikwa.
#Hadi sasa ukarabati wa barabara ya Ubena Zomozi hadi kuelekea katika mradi wa Stiegler's Gorge umefikia asilimia 50 - Mhe. Kwandikwa.
#Mradi wa REA III unaoendelea katika Mkoa wa Mwanza unategemewa kukamilika Juni, 2019 - Mhe. Subira Mgalu.
#Redio ya mezani kwa ajili ya Kituo cha Polisi Jozani imeshapatikana na mafundi wa redio za Polisi wanamalizia ufungaji wake ili kurejesha mawasiliano ya uhakika - Mhe. Masauni