Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara ya Mifugo na Uvuvi Yatoa Vitendea Kazi vya Mazao ya Mifugo
May 29, 2020
Na Msemaji Mkuu

Na Prisca Libaga, Maelezo / Arusha.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa vitendea kazi vya mazao ya mifugo kwa wachunaji wa ngozi kwenye machinjio yote ya Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa ngozi.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha kwa niaba ya wachunaji hao, Mkurugenzi wa Masoko na Uzalishaji, Felix Nandonde alisema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa zikiharibiwa ubora wake kwa matumizi ya vifaa visivyo na ubora.

Kwa mujibu wa Nandonde wizara ilitoa mafunzo ya siku moja kwa wachunaji wa ngozi wa mkoa huo ili kuboresha thamani ya ngozi ikiwemo kutoa leseni kwa kila mchunaji na vifaa hivyo kwa lengo la kuongeza ubora kwenye kazi zao.

Baadhi ya vitendea kazi hivyo ni visu vya kisasa ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa na wamepanga kuvitoa kwa wachunaji wa mkoa wa Arusha na nchini kwa ujumla.

“Kwa kipindi kirefu sekta ya uchunaji nchini imekuwa ikionekana haina mwenyewe lakini sasa kupitia Serikali ya Awamu ya Tano imeanza kutambulika kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo”, Alisema Nandonde.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, David Lyamongi, aliipongeza wizara hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wachunaji pamoja na vitendea kazi hivyo.

Wizara ya mifugo na Uvuvi imetoa vitendea kazi hivyo kwa wachunaji wa ngozi kwenye machinjio yote ya mkoa huo kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa ngozi.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo kwa niaba ya wachunaji Mkurugenzi Nandonde alisema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa zikiharibiwa ubora wake kwa matumizi ya vifaa visivyo na ubora.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi