Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

WIZARA YA HABARI NA TPSF KUONGEZA USHIRIKI KONGAMANO LA KISWAHILI UFARANSA
May 13, 2026
WIZARA YA HABARI NA TPSF KUONGEZA USHIRIKI  KONGAMANO LA KISWAHILI  UFARANSA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, akizungumza na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Deogratius Massawe pamoja na watumishi wa wizara kuhusu Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili litakalofanyika jijini Paris, Ufaransa, kuanzia tarehe 4 hadi 7 Julai 2026.
Na Mwandishi Wetu

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amesema, Kongamano la Kiswahili linalotarajiwa kufanyika  nchini Ufaransa linatoa fursa kwa Sekta  Binafsi nchini kutangaza biashara, huduma na fursa zilizopo Tanzania ili kuvitia washirika na wawekezaji wapya.


Msigwa amesema hayo wakati alipokutana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Deogratius Massawe, tarehe 13 Mei, 2026 Jijini Dar es Salaam kujadili ushiriki wa sekta binafsi katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili litakalofanyika jijini Paris, Ufaransa, kuanzia tarehe 4 hadi 7 Julai 2026.

Amesema ushiriki huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kutumia Kiswahili kuimarisha diplomasia ya kiuchumi ambapo kwa kutumia jukwaa hilo wataweza kutangaza bidhaa, huduma na fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.

 

"Kiswahili kitatumika kama daraja la mawasiliano kuvutia wawekezaji na washirika wapya kutoka Ufaransa na mataifa mengine,” alisisitiza Msigwa.

Kwa upande wake, Massawe ameahidi kuwa TPSF itahakikisha wafanyabiashara na wawekezaji wanachangamkia fursa hiyo ili kunufaika kiuchumi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi

slot gacor