Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara ya Ardhi Yapata Tuzo katika Kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Sep 20, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata Cheti na Tuzo katika Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushika nafasi ya tatu kwa upande wa kundi la Wizara.

Tuzo hiyo imekabidhiwa jana Septemba 19, 2022 wakati wa Kongamano la Sita la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi lililofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano.

Katika kongamano hilo Waziri Mkuu aliwataka wadau wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kuongeza nguvu katika kutoa huduma za uwezeshaji hasa maeneo ya pembezoni ya miji na vijijini ili kufikia malengo ya nchi katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Aidha, aliitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuongeza kasi katika kupima na kurasimisha maeneo mbalimbali nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi