Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wizara Haitaingia Mkataba na Mtoa Huduma Binafsi Asiye na Kiapo cha Uadilifu - Dkt. Abbasi
Feb 07, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50776" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na watumishi wa Wizara hiyo leo jijini Dodoma, ambapo aliwasisitiza kufanya kazi kwa bidii, kizalendo na kwa ushirikiano ili kufikia malengo ya Serikali.[/caption]

Na Anitha Jonas – WHUSM

07/02/2020, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa wizara haitaingia mkataba na mtoa huduma yoyote wa sekta binafsi ambaye hajasaini kiapo cha uadilifu na BRELA.

Dkt.Abbasi ametoa tamko hilo leo Jijini Dodoma, alipokuwa akifanya kikao na Watumishi wa Wizara mara baada ya kuapishwa kwa lengo la kuzungumza na watumishi na kutoa maelekezo ya utekelezaji wa majukumu ambapo amesisitiza kuwa sekta zote za wizara ni nguvu laini ya nchi (soft power).

"Katika semina hii ya kiapo cha uadilifu tumejifunza kuwa watoa huduma wote kutoka sekta binafsi wanapokuwa wanaingia mikataba na serikali wanapaswa wawe wamesaini kiapo cha uadilifu na BRELA pia waweke uthibitisho wa kiapo hicho kwenye mkataba na katika kusimamia kiapo hichi nasisitiza uadilifu kwa watumishi,uzalendo na uwajibikaji," alisema Dkt.Abbasi.

[caption id="attachment_50777" align="aligncenter" width="750"] Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa kikao kilichofanyika leo Jijini Dodoma[/caption] [caption id="attachment_50779" align="aligncenter" width="750"] Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakila kiapo cha Uadilifu katika utumishi wa umma baada ya Semina elekezi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiwa ni Sehemu ya Kikao kazi cha watumishi wa Wizara hiyo.[/caption] [caption id="attachment_50780" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi[/caption]

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo wa wafanyakazi Katibu Mkuu huyo alisisitiza mambo mbalimbali kwa wafanyakazi ikiwemo umuhimu wa kuchapa kazi kwa kuzingatia muda pamoja na kuacha majungu kazini na ugoigoi.

Naye Kaimu Katibu Msaidizi Sekretariaeti ya Maadili kwa Umma Kanda ya Kati Bibi. Bibi.Jasmine Bakari alifafanua kuwa utaratibu wa kiapo cha ahadi ya uadilifu hufanyika katika vipindi mbalimbali  ikiwemo pale kiongozi anapobadilishwa, hivyo watumishi hutakiwa kutoa ahadi ya kiapo cha uadilifu kwa kiongozi huyo.

"Semina tuliyotoa leo katika wizara hii ni sehemu ya majukumu ya taasisi  yetu na tumekuwa tukifanya hivi kwa lengo la  kuwakumbusha watumishi wa umma kuhusu kiapo cha uadilifu katika utendaji,"alisema Bibi.Jasmine.

Halikadhalika nae mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo kutoka Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bi.Happiness Kalokola alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kikao alichokifanya pamoja na mafunzo yaliyotolewa kwani  yamesaidia kuwakumbusha watumishi suala la uadilifu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi