Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Wakagua Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere
Oct 12, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Nishati, January Makamba pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato wamekagua kazi mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere unaotekelezwa wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.Ukaguzi huo umefanyika kabla ya ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdory Mpango katika mradi huo itakayofanyika tarehe 12 Oktoba, 2021.

Katika ukaguzi huo, viongozi hao waliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Felchesmi Mramba, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila na watendaji wengine kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na kutoka mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP).

Maeneo waliyokagua ni pamoja Tuta Kuu la Bwawa, njia za kupeleka maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme, Jengo la mitambo pamoja, kituo cha kupokea na kusafirisha umeme pamoja na ujenzi wa daraja la kudumu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi