Sehemu ya Washiriki wa Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia Kampeni ya Kili Challenge.
Washiriki wengine katika kampeni hiyo wametumia Baiskeli kuzunguka Mlima Kilimanjaro.
Kiongozi wa wapandaji ,Bw Moses kutoka mgodo wa dhahabu wa Geita akipokelewa na Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu mara baada ya kushuka kutoka katika kilele cha Uhuru.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu akikabidhi vyeti kwa mshiriki aliefanikiwa kufika katika Kilele cha Uhuru.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa zoezi la kupanda Mlima.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa zoezi la kuzunguka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia baiskeli.