Waziri Nape Azindua Huduma za Mawasiliano ya Intaneti ya Kasi kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro
Dec 09, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati akizindua huduma za mawasiliano ya intaneti ya kasi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro leo Desemba 09, 2022 hafla ambayo imefanyika kwenye Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA). Baada ya uzinduzi huo Waziri Nape amewaongoza viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo wakiwemo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuelekea kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuhitimisha uzinduzi huo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizindua huduma za mawasiliano ya intaneti ya kasi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro leo Desemba 09, 2022 hafla ambayo imefanyika kwenye Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA). Baada ya uzinduzi huo Waziri Nape amewaongoza viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo wakiwemo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuelekea kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuhitimisha uzinduzi huo.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akishuhudia wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kiutendaji kati ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Tukio hilo limefanyika leo Desemba 09, 2022 wakati wa Uzinduzi wa Huduma za Mawasiliano ya Intaneti ya Kasi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro hafla ambayo imefanyika kwenye Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).