Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mwakyembe Aipongeza Timu ya Serengeti Boys kwa Kuitangaza Tanzania.
May 26, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_1663" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimpa mkono wa kumkaribisha nyumbani mchezaji wa Serengeti Boys Bw. Abdul Sulemani (kushoto) katika hafla ya kuwapokea wachezaji hao waliorejea nchini kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Shamimu Nyaki.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, ameipongeza timu ya vijana chini ya miaka 17 “Serengeti Boys” kwa hatua nzuri  waliyofikia katika kiwango cha Soka la Afrika kwa kushika nafasi ya pili katika kundi B walilokuwa wanacheza wakati wa michuano ya AFCON iliyomaliziki hivi karibuni Mjini Gabon.

Pongezi hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuipokea timu hiyo, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, ambapo Waziri Mwakyembe aliwataka walimu na wachezaji  hao  kuendelea kujiandaa kwa ajili ya mashindano mengine yaliyo mbele yao.

“Nimefurahi kwa hatua mliyoifikia na watanzani wote wanawapongeza, kwa kuwa mmeshindana kwa uwezo wenu na kuirudisha Tanzania katika ramani  ya soka, baada ya kukaa nje ya michezo ya AFCON  kwa takribani miaka 30 alisema” Mhe Mwakyembe.

Aidha aliongeza kuwa hapo walipofika Serengeti Boys ni mashujaa na Serikali inaahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa  vipaji hivyo vinaendelezwa kwa ajili ya ngazi nyingine za kisoka.

[caption id="attachment_1664" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Serengeti Boys pamoja na viongozi wa timu hiyo katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kurejea kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1666" align="aligncenter" width="750"] Wachezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 17 “Serengeti Boys” wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kurejea kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Naye Kocha wa Serengeti Boys Kim Paulsen ameiomba Serikali na wadau wa michezo nchini kuendelea kuisadia  timu hiyo katika maandalizi mbalimbali ili kuipa motisha zaidi katika kufanikisha ndoto ya Tanzania katika mchezo wa soka.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya Serengeti Boys Dickson Job amewashukuru watanzania  kwa mchango  mkubwa walioutoa kwao katika maandalizi mpaka hapo walipofikia ingawa hawakufanikiwa kurudi na ushindi.

“Mchezo una matokeo matatu kushinda, kushindwa au kutoka sare ingawa hatukutarajia kushindwa kwa kuwa tulitamani sana kurudi na ushindi  kama ambavyo tuliwaahidi watanzania ila mwaka huu bahati haikuwa yetu, ila tunaahidi kuendeleza mapambano katika hatua zijazo” alisema nahodha huyo.

Timu ya Serengeti Boys imerejea nyumbani baada ya kumalizika kwa michuano ya AFCON ambapo watapumzika na kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na michuano inayofuata ya  vijana chini ya miaka 20 inayounda timu ya Ngorongoro Heroes.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi