Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mulamula Ateta na Mabalozi wa Ufaransa, Italia na Uswisi
Apr 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini, Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Didier Chasot katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana kwa pamoja na kufanya mazungumzo na mabalozi wa Ufaransa, Italia na Uswisi.

Waziri Mulamula amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini, Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Didier Chasot katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira.

Balozi wa Uswisi nchini, Mhe. Didier Chasot (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri Mulamula amewahakikishia mabalozi hao kuwa Serikali ipo tayari wakati wote kushirikiana na nchi zao katika utunzaji wa mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi (mwenye suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati wa mazungumzo yao

“Serikali ya Awamu ya Sita imetoa kipaumbele katika utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema Balozi Mulamula.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini, Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Didier Chasot. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme na Afisa kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba.  

Nae Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Hajlaoui kwa niaba ya mabalozi wengine, amesema wanafurahishwa na jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na utunzaji wa mazingira. 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi