Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu: Wezi wa Nondo Tani 5 Wasakwe Mara Moja
Jul 19, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45435" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na Viongozi, Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Sekretarieti ya Mkoa, katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Julai 18.2019.[/caption]

*Ni za ujenzi wa kituo cha kimataifa cha mabasi cha Moshi

*RPC athibitisha watu watano wamekamatwa kufuatia agizo hilo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah awasake na kuwatia mbaroni watu waliohusika na wizi wa tani tano za nondo na kisha wakatoroka.

Alitoa agizo hilo jana jioni, (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizungumza na wafanyakazi na wananchi mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Moshi, katika kata ya Ngangamfumuni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi za siku nne, alisema mradi huo ni maalum kwani uko miongoni mwa miradi ambayo Serikali imekuwa ikiweka utaratibu wa kupelekea fedha kwenye miradi iliyotengwa na Halmashauri.

[caption id="attachment_45437" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia ramani ya ujenzi wa stendi mpya ya Ngangamfumuni, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa, mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.[/caption] [caption id="attachment_45438" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mradi wa ujenzi ya stendi mpya ya Ngangamfumuni, wakati alipokagua mradi huo, uliyopo katika Halmashauri ya Manispaa, mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019.[/caption]

“Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 9 za kuanzia mradi huu lakini inasikitisha kuona kwamba wanaMoshi mnahujumu kwa kuiba vifaa vya ujenzi. Ninazo taaarifa kuwa hapa zimeibiwa tani tano za nondo na zimeshakamatwa.”

“Ni aibu, ni aibu kwa wana-Moshi. Ninyi wenyewe mnauhujumu huu mradi. Manispaa iweke utaratibu wa ulinzi ili vifaa vingine visipotee zaidi. Mkuu wa Wilaya chukua hatua ya kuwafuatilia wote waliohusika,” alisema.

Kupitia maswali aliyouliza, Waziri Mkuu alibaini kuwa walinzi wawili waliokuwepo siku ya tukio walitoroka ndipo akaamua kumwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa, awasake na kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ujenzi wa stendi hiyo kubwa unafanywa na mkandarasi mkuu ambayo ni kampuni ya CRJE ya China akishirikiana na wakandarasi wasaidizi watano na unatarajiwa kukamilika Januari 2021. Hadi kukamilika, ujenzi huo unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 28.8.

[caption id="attachment_45439" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua mradi wa ujenzi ya stendi mpya ya Ngangamfumuni, iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa, mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).[/caption]

Ikikamilika, stendi hiyo ambayo itakuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka. Kati ya hayo, mabasi 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20.

Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kukamatwa kwa watu watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na wizi wa tani tano za nondo katika eneo la ujenzi wa stendi hiyo lililopo Ngangamfumuni.

“Hawa watu tumewakamata jana jioni, na kati ya walinzi waliotoroka, tumemkamata mmoja wao tayari akiwemo mkazi wa Rau, Daudi Audifasi mwenye miaka 48 ambaye anadaiwa kutoboa ukuta wa uzio kwa chini, na kukutwa na nondo nyumbani kwake ambako ni mita 10 kutoka eneo la tukio.”

Amesema tukio hilo, lilitokea Julai 6, mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi ambapo walinzi wa eneo hilo ambao ni Maxshield company walitoroka baada ya tukio hilo. Kamanda Issah alithibitisha kwamba nondo hizo zimekamatwa na ziko polisi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi