Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu wa Ethiopia Atua Nchini kwa Ziara ya Kitaifa
Feb 29, 2024
Waziri Mkuu wa Ethiopia Atua Nchini kwa Ziara ya Kitaifa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali akikaribishwa nchini na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba baada ya kuwasili leo tarehe 29 Februari, 2024 kuanza ziara yake ya kitaifa ya siku tatu.
Na Mwandishi wetu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali amewasili nchini leo tarehe 29 Februari 2024 kuanza ziara yake ya  kitaifa ya siku tatu.


Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Waziri Mkuu Abiy amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba.


Mhe. Dkt. Abiy atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 01 Machi 2024.


Pamoja na mambo mengine ziara ya Waziri Mkuu Abiy inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafirishaji kwa njia ya anga, nishati, kilimo na mifugo, biashara na uwekezaji na Ushirikiano katika sekta za elimu, uhamiaji, na ulinzi na usalama


Ziara hiyo ambayo itakamilika tarehe 02 Machi 2024 inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi