Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu: Mradi wa Barabara Chamwino Ni Alama ya Kudumu kwa Wananchi
Apr 13, 2026
Waziri Mkuu: Mradi wa Barabara Chamwino Ni Alama ya Kudumu kwa Wananchi
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Ntyuka–Mvumi–Kikombo yenye urefu wa kilomita 76 pamoja na kipande cha barabara ya Chololo–Mapinduzi, chenye urefu wa kilomita 5 leo April 13, 2026, jijini Dodoma
Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara katika Wilaya ya Chamwino ni sehemu ya dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwaachia alama ya kudumu wakazi wa eneo hilo kupitia miradi ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara hizo, Dkt. Nchemba amesema barabara hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi, hasa kwa kuwa eneo hilo ni kitovu cha uzalishaji.

“Utekelezaji wa mradi huu ni dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kuwaachia alama ya kudumu wakazi wa eneo hili. Hii ni barabara muhimu sana kwa kuwa nimepita na kuona hili ni eneo la uzalishaji,” amesema Dkt. Nchemba.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alikuwa akikagua ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Ntyuka–Mvumi–Kikombo yenye urefu wa kilomita 76 pamoja na kipande cha barabara ya Chololo–Mapinduzi, chenye urefu wa kilomita 5.

Mradi huo unatekelezwa katika Jimbo la Mvumi, Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, na unatarajiwa kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi