Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Majaliwa Ahani Msiba wa Rais Mstaafu Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi
Mar 06, 2024
Waziri Mkuu Majaliwa Ahani Msiba wa Rais Mstaafu  Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na kutoa mkono wa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipofika Ikulu Migombani Wilaya ya Mjini Uguja jijini Zanzibar kwa kufiwa na baba yake mzazi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijiji kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
Na Ikulu - Zanzibar

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi alipofika Ikulu Migombani Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kifo cha baba mzazi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofika Ikulu Migombani kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuhani msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, baada ya kumaliza kutoa mkono wa pole kufuatila kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Ahajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi