Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atoa Maelekezo kwa Maafisa Ugani
Jul 12, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33469" align="aligncenter" width="938"] Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa alipowasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango kwa ajili ya kukutana na Maafisa Ugani wa nchi nzima leo Jijini Dodoma.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.[/caption]

*Awataka Wasimamie Mifumo Rasmi ya Ununuzi wa Mazao

Na: Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ofisi za maafisa ugani zinapaswa kuwepo walipo wakulima, wafugaji na wavuvi na kwamba maafisa ugani katika ngazi zote lazima wawezeshwe na wasimamiwe kikamilifu.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Alhamisi, Julai 12, 2018) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa maafisa kilimo, mifugo na uvuvi kutoka Tanzania Bara ulioanza leo kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma. Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki 570.

“Maafisa ugani katika ngazi zote lazima wawezeshwe na wasimamiwe kikamilifu kutekeleza majukumu yao. Wataalam wa Wizara washuke hadi ngazi ya mikoa na Halmashauri kusaidiana na waliopo kwenye ngazi hizo.

  [caption id="attachment_33470" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Tixon Nzunda akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa alipowasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango kwa ajili ya kukutana na Maafisa Ugani wa nchi nzima leo Jijini Dodoma. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo.[/caption] [caption id="attachment_33471" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akitoa maelekezo kwa Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati akifungua kikao cha maafisa hao leo Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Magumba na Naibu Katibu Mkuu - TAMISEMI, Dkt. Tixon Nzunda.[/caption] [caption id="attachment_33472" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akitoa maelekezo kwa Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati akifungua kikao cha maafisa hao leo Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Magumba na Naibu Katibu Mkuu - TAMISEMI, Dkt. Tixon Nzunda.[/caption]

“Walioko ngazi ya mkoa washuke mara kwa mara hadi ngazi ya Halmashauri na ngazi ya Halmashauri ishuke na kushirikiana na maafisa ugani wa kata na vijiji kuelekeza wakulima, wafugaji na wavuvi kuhusu utaalam na maarifa yanayohitajika katika kuendeleza sekta hizi kibiashara,” amesema.

Amesema wakulima, wafugaji, na wavuvi hawana budi kupatiwa mbinu bora kuanzia hatua ya uzalishaji hadi kupata masoko ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia sahihi zenye tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Amesisitiza kwamba maafisa ugani ni lazima wawe na orodha sahihi ya wakulima, wafugaji na wavuvi wote kuanzia ngazi ya kitongoji na aina ya mazao wanayoshughulikia, malengo ya uzalishaji na utekelezaji.

[caption id="attachment_33473" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza katika kikao baina ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wapili kulia) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Magumba na Naibu Katibu Mkuu - TAMISEMI, Dkt. Tixon Nzunda.[/caption] [caption id="attachment_33474" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza katika kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption] [caption id="attachment_33475" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba akizungumza katika kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wapili kulia) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption]

“Maafisa ugani wawe na takwimu sahihi za aina na kiasi cha mahitaji ya teknolojia na  pembejeo za uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi katika maeneo yao lakini pia wasaidie kuunganisha vikundi vya wakulima, wafugaji, wavuvi na kuunda ushirika imara ili kuendeleza juhudi za kufufua ushirika kama mkombozi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.”

“Ukiwa na ushirika imara hata kama unataka kuwapatia taarifa ya haraka kuhusu ongezeko la bei, au tarehe ya mnada inakuwa rahisi kwa sababu wana Mwenyekiti wao au Katibu wao na kupitia kwake, wote wanaweza wakaitishwa na kupewa taarifa kwa haraka,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka maafisa ugani waende wakasimamie mifumo rasmi ya ununuzi wa mazao ili kuwasaidia wakulima kupata bei nzuri za mazao yao.

[caption id="attachment_33476" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akizungumza katika kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption] [caption id="attachment_33477" align="aligncenter" width="1000"] Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayosimamia Maendeleo ya Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT), Geoffrey Kirenga akitoa salama kwaniaba ya wadau wa sekta ya kilimo katika kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (watatu kulia) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption] [caption id="attachment_33478" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Tixon Nzunda akizungumza katika kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa nne kulia) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption]

“Hatutaki kusikia watu wanatumia mifumo isiyo rasmi kama chomachoma (kwenye ufuta), butura (kahawa huko Karagwe), katakichwa (kahawa Moshi), kangomba (korosho) na vishada (tumbaku). Nenda kapambane nao, wewe ni afisa wa Serikali na hupaswi kuacha wananchi wanateseka,” alisema.

“Nenda kahimize mfumo wa kuuza mazo kwa ushirika badala kuruhusu wanunuzi kwenda kwa mkulima mmojammoja. Pia mtusaidie kufafanua dhana ya Stakabadhi za mazao Ghalani kwamba siyo malipo ya papo kwa papo. Muwaeleze wakulima kwamba wanapeleka mazao pake wakati wakisubiria bei iwe nzuri, siyo kwamba wanakopwa,” amesisitiza.

[caption id="attachment_33479" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Uratibu wa Idara za Kisekta toka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Andrew Komba akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption] [caption id="attachment_33481" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya washiriki wa kikao baina ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) na Maafisa Ugani kutoka katika Halmashauri zote nchini wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.[/caption] [caption id="attachment_33482" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya washiriki wa kikao baina yake na Maafisa Ugani kutoka Halmashauri zote nchini mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 12 Julai, 2018 Jijini Dodoma. Takribani maafisa Ugani 700 wanakutana kwa siku mbili Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kupanga mipango ya uboreshaji wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi. (Picha zote na: Frank Shija)[/caption]

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. Selemani Jafo alisema Aprili mwaka huu, Serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji wa agizo la kuwa na viwanda 100 kwa kila mkoa na kubaini kuwa umefikia 49.4 ndani ya miezi mitatu tu.

“Tarehe 20 Aprili, 2018, tulifanya kikao cha kwanza cha utekelezaji wa wa agizo la kila mkoa uhakikishe unajenga viwanda 100 vidogo na vya kati. Kwenye agizo hilo, tulilenga malighafi za viwanda hivyo zitokane na mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo. Agizo hilo lilitaka wakuu wa mikoa wawe wamelitekeleza kati ya Desemba 2017 na Desemba 2018; na kufikia Aprili 2018, viwanda 1,280 vilikuwa vimeshajengwa sawa na asilimia 49.4 ya lengo tulilojiwekea,” alisema.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi