Waziri Mkuu Azindua Tamasha la Kitaifa la Utamaduni
Jul 02, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Kwanza la Kitaifa la Utamaduni wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua tamasha hilo kwenye uwanja wa Uhuru, Temeke mkoani Dar es salaam, Julai 2, 2022.
Wasanii kutoka Mkoa wa Mwanza wakicheza ngoma ya nyoka katika Tamasha la Kwanza la Kitaifa la Utamaduni lililofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Uhuru, Temeke jijini Dar es slaam, Julai 2, 2022.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua Kitabu Cha Muongozo wa Maadili na Utamaduni wa Mtanzania muda mfupi baada ya kuzindua pia Tamasha la kwanza kitaifa la Utamaduni leo Julai 02, 2022, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua Mabanda ya Vikundi mbalimbali vya Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar vilivyoshiriki Tamasha la kwanza kitaifa la Utamaduni linalofanyika leo Julai 02, 2022, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, baada ya kuzindua rasmi Tamasha hilo. Katika ukaguzi huo aliambatana na Waziri, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu, Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na viongozi wengine .