Waziri Mkuu Azindua Huduma Mpya za Fedha Kidigitali, Teleza Kidigitali.
Apr 11, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa huduma mpya za fedha ambazo zitatolewa kidigitali na Benki ya NMB “Teleza Kidigitali” katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma, Aprili 11, 2022. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hassan Hamad Chande, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya za fedha ambazo zitatolewa kidigitali na Benki ya NMB “Teleza Kidigitali” katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma, Aprili 11, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya za fedha ambazo zitatolewa kidigitali na Benki ya NMB “Teleza Kidigitali” katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma, Aprili 11, 2022.