Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Soko la Kisasa Tarime Mjini
Feb 29, 2024
Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Soko la Kisasa Tarime Mjini
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua kitambaa kuashiria ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji Tarime, wakati wa ziara yake mkoani Mara, Februari 28, 2024. Soko hilo limegharimu shilingi bilioni 9.68.
Na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa soko la kimkakati la Tarime mjini unaotarajiwa kugharimu shilingi bilioni 9.6 hadi kukamilika kwake.

 

Akipokea taarifa ya ujenzi wa soko hilo jana jioni (Jumatano, Februari 28, 2024), Waziri Mkuu alielezwa kwamba mradi huo kwa sasa upo katika hatua ya umaliziaji na umefikia asilimia 82 ya utekelezaji.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji Tarime baada kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, wakati wa ziara yake mkoani Mara, Februari 28, 2024. Soko hilo limegharimu shilingi bilioni 9.68.

Akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime, Bi. Gimbana Ntavyo alisema shughuli zinazoendelea kwa sasa ni skimming, upakaji wa rangi, ufungaji wa milango kwenye maduka na vyoo na ufungaji wa mifumo ya umeme na maji kwenye jengo kuu la soko.

 

Alisema kazi nyingine ni uwekaji wa vigae na terazo kwenye vizimba, maduka ya nje na ndani na kwa upande wa kazi za nje, wanaendelea na uzalishaji wa paving na kuandaa maeneo ya kuzipanga.

 

Muonekano wa soko la kisasa katika Halmashauri ya Mji Tarime ambalo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, wakati wa ziara yake mkoani Mara, Februari 28, 2024. Soko hilo limegharimu shilingi bilioni 9.68.

“Hadi sasa malipo yaliyofanyika kwa mkandarasi ni shilingi bilioni 5.77 na kwa mshauri ni shilingi milioni 120.36 sawa na asilimia 60.86 ya gharama za mradi,” alisema na kuongeza: “Mradi huu utakuwa na maduka 325, vizimba 160, mabucha matatu, migahawa miwili, supermarket moja na Benki mbili.”

 

Akielezea manufaa ya mradi huo, Mkurugenzi huyo alisema mradi huo umetoa ajira za muda kwa watu 441 na utakapokamilika halmashauri inatarajia kuongeza mapato yake ya ndani kwa shilingi milioni 588 kwa mwaka kutokana na mapato yatakayokusanywa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi