[caption id="attachment_7528" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.[/caption]
Na. Paschal Dotto
Vyuo vikuu vilivyofungiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018 vimetakiwa kukamilisha matakwa yanayohitajika kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya vyuo vikuu nchini yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini, Dar es Salaam.
[caption id="attachment_7529" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu toka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila (kushoto) akitoa neno la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_7534" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Vyuo Vikuu nchini Prof. Jacob Mtabaji (kushoto) akitoa neno la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.[/caption]“Vyuo vikuu vyote nchini vinatakiwa kutoa elimu bora kwa wahitimu ili kuwawezesha kujiajiri na kuendana na Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Tanzania yenye viwanda,” amesema Majaliwa.
Majaliwa ameongeza kuwa, ili kujenga uchumi wa viwanda vyuo vikuu hapa nchini vinatakiwa kufundisha na kuwawezesha wahitimu kujiajiri ili kuendana na ushindani katika soko la ajira kitaifa, kimataifa na Dunia kwa ujumla.
Vile vile vinatakiwa kukuza stadi katika sekta ya viwanda kwa kupata wasomi waliofundishwa kwa vitendo kutoka katika vyuo mbalimbali, kuweka mikakati na kuboresha elimu ili kuendana na dhamira ya Serikali pamoja na kuweka mitaala mizuri kwa wanafunzi katika vyuo hivyo ili kuendana na mabadiliko yaliyofanywa katika udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
[caption id="attachment_7537" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_7540" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.[/caption]Aidha Majaliwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa bajeti Shilingi Tril. 4.7 kwa Wizara ya Elimu ili kuboresha elimu ambayo itahusisha katika kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu hapa nchini ikiwemo mikopo ya elimu ya juu na mahitaji mengine ya vitabu kwa shule za Sekondari.
Naye Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amevitaka vyuo vikuu hususani vile vilivyofungiwa kwa kutokidhi matakwa ya utoaji elimu hapa nchini, kukaa na kuweka mambo sawa ili waweze kufanyiwa uhakiki upya na TCU.
[caption id="attachment_7541" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu Nelson Mandela wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_7543" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo ya namna ya kujiunga na vyuo vikuu wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa)[/caption]“Ili chuo kiweze kukamilika kutoa elimu bora lazima kiwe na miundombinu bora, wahadhili waliobobea, mitaala safi, wanafunzi wenye sifa na kujituma,” amefafanua Mwijage.
Maonesho hayo ni ya 12 tangu yalivyoanzishwa mwaka 2005 ambapo kwa mwaka huu zaidi ya vyuo vikuu 80 kutoka ndani na nje ya nchi vinashiriki. Maonesho yatafanyika kwa siku Nne kuanzia Julai 26 hadi Julai 29 mwaka huu.