Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Atembelea Maonesho ya Nanenane Uwanja wa John Mwakangale Mbeya
Aug 03, 2023
Waziri Mkuu Atembelea Maonesho ya Nanenane Uwanja wa John Mwakangale Mbeya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama miche ya parachichi wakati alipotembelea banda la kikundi cha Chilongola Agro Ferest cha Mafinga mkoani Iringa katika maonesho ya wakulima ya Kimataifa Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 3, 2023. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na kulia kwa Waziri Mkuu ni mlezi wa kikundi hicho na Mbunge wa viti maalum Iringa, Ritta Kabati.
Na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mafuta ya kula yaliyotokana na alizeti wakati alipotembelea banda la Wilaya ya Chunya katika maonesho ya Wakulima ya Kimataifa Nanenane kwenye uwanja  wa John Mwakangale jijiii Mbeya, Agosti 3, 2023.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ufugaji wa kisasa wa samaki aina ya Sato wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya wakulima  ya kimataifa Nanenae kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya, Agosti 3, 2023. Kushoto kwake ni Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

 

 

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama zabibu zilizokaushwa bila kupoteza virutubisho wakati alipotembelea banda la Wilaya ya Chunya katika Maonesho ya Wakulima ya Kimataifa Nanenane kwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya, Agosti 3, 2023.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama fuvu la tembo wakati alipotembelea banda la maonesho la Wilaya ya Chunya katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 3, 2023. 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi