Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri mkuu Ataka Vyombo vya Ulinzi Kuimarisha Mshikamano sekta ya Madini
Jan 26, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50463" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofunga semina ya Viongozi wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini kwenye ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma, Januari 26, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Aipongeza Wizara ya Madini[/caption]

Asteria Muhozya, Greyson Mwase Tito Mselem, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim  Majaliwa amevitaka Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuimarisha mshikamano ili mwenendo wa usimamizi wa rasilimali madini uimarishe uchumi.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Januari 26 wakati akifunga rasmi Semina ya Siku mbili kuhusu Ushiriki wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali madini iliyofanyika jijini Dodoma na kuvishirikisha vyombo hivyo kutoka mikoa yote nchini pamoja na baadhi ya wadau wa madini.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amevitaka vyombo hivyo kutumia weledi na utashi kuhakikisha vinaweka mazingira bora katika maeneo yao yatakayowezesha kuvutia wawekezaji kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kuifungamanisha na sekta nyingine.

Pia, amewataka Maafisa Madini kote nchini kuimarisha ushirikiano na vyombo hivyo pamoja na wadau wa madini walioko katika maeneo yao ili kuwezesha shughuli za madini kutelekelezwa kikamilifu.

Katika hatua nyingine, amevitaka vyombo hivyo kuacha matumizi ya lugha za jazba na zinazokatisha tama pindi inapotokea changamoto na kuvitaka kutoa nafasi za kujieleza ili kuendelea kuwatia moyo wawekezaji.

 ‘’ Hatutaki kuona wawekezaji wanatuibia lakini kuna njia zinazofaa kuchukuliwa wakati wa kushughulikia masuala haya. Tumieni sheria, kanuni na miongozo mahususi iliyowekwa katika kusimamia sekta hii,’’ amesisitiza Waziri Mkuu.

Aidha, amevitaka vyombo hivyo kujenga mazingira rafiki ya kazi, kuaminiana na kufanyakazi kwa umoja na ushirikiano huku vikipaswa kutambua na kuheshimu nafasi na taaluma za wengine na akasisitiza ushauri kutumika katika kutatua changamoto.

Vilevile, Waziri Mkuu ameipongeza Wizara ya Madini kutokana na kusimamia sekta ya madini   kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta na kuzifanyia kazi ikiwemo usimamizi wa ukusanyaji mapato na kueleza kuwa, imekuwa mfano mzuri katika kuongeza tija na kwamba matokeo yanaonekana.

Akizungumzia masoko ya madini, ametaka wadau wote wa sekta hiyo nchini kuhakikisha wanayatumia na kusisitiza yale yanayosafirishwa kwenda nje kupita sokoni huku yale yanayoingizwa ndani ya nchi, kuhakikisha yanaanzia sokoni.

Kuhusu uwajibikaji wa kampuni za madini kwa jamii, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita kutokana na kusimamia michango inayotolewa na kampuni ya Madini ya Geita (GGM)ambayo imechangia Bilioni 10 hali iliyowezesha maendeleo ya kijamii mkoani humo ikiwemo ujenzi wa zahanati na kuwataka watendaji wengine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko ameweleza Waziri Mkuu kuwa, bado ipo changamoto ya madini bandia ambayo baadhi ya watanzania ambao kwa kutumia viwanda vyao wamekuwa wakitengeneza madini hayo na kuwaeleza kuwa, ‘’serikali itaweka mkakati maalum kuhakikisha suala hilo halifanyiki Tanzania’’.

Mhe. Waziri Mkuu zama za biashara ya haramu na madini bandia sasa ni zilipendwa, kwa kushirikiana na vyombo hivi tutahakikisha madini hayo zama za biashara haramu   zinakwisha nchini,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Akizungumzia semina hiyo, Waziri Biteko amemweleza Waziri Mkuu kuwa ni hatua ya mwanzo ya kujenga mazingira ya kuvutia mitaji ya uwekezaji katika sekta ya madini kutoka ndani na nje ya nchi na  kwamba kukutana huko kumesaidia kujenga uelewa wa pamoja katika kuimarisha usimamizi wa sekta ya madini.

Semina hiyo ni ya kwanza kufanyika nchini kati ya Wizara ya Madini na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi