Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Aipongeza NHC kwa Utendaji
Jul 14, 2017
Na Msemaji Mkuu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi. Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole, Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa na Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na. Mwandishi Wetu.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.

Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa ulianza mwezi Machi mwaka huu na sasa tayari imekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo ya jirani.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana jioni wakati akizugumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akikagua kifaa katika Zahanati ya Mnolela baada ya kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi. Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza  huduma karibu kwa wananchi wake.

“Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono”, alieleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu shilingui milioni 65.5.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi. Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, shilingi milioni 10 zilitolewa na Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri”, alieleza Mchechu.

Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape Nnauye alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Mnauye alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo  akiwa njiani kuelekea Lindi. Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakazi wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi