Waziri Mhe. Jamal Akutana na Kuzungumza na Waziri Mhe. Dkt. Stergomena Tax
Nov 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali, alipofika Ofisini kwake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Ikulu Jijini Zanzibar leo 17-11-2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali akiagana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Ikulu Jijini Zanzibar leo 17-11-2022.