Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mhagama Awataka Wananchi Kuondoka Maeneo Hatarishi
Apr 12, 2024
Waziri Mhagama Awataka Wananchi Kuondoka Maeneo Hatarishi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akizungumza na kuwafariji wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.
Na Tegemeo Kastus

Wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wamefanya ziara ya kutembelea Mradi wa Hifadhi Endelevu ya Ardhi katika Bonde la ziwa Nyasa (SLM-Nyasa) unaotekelezwa na ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Machi 16, 2024.

 

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Jackson Kiswaga, wajumbe hao wamekagua moja ya boti za injini za uvuvi zilizotolewa kwa vikundi vya wavuvi katika ziwa Nyasa ili kuwawezesha kujipatia kipato pasipo kuharibu mazingira.

 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kiswaga amesema kamati imeridhishwa na mradi huo na kuishukuru Serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuratibu mradi huo ambao umeleta manufaa kwa wananchi na hifadhi ya mazingira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima walipotembelea na kuwafariji wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis aliyeambatana na kamati hiyo ameendelea kuwahimiza wananchi kuitunza miradi hiyo.

 

Mradi wa SLM–Nyasa unalenga kuwajengea wananchi uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha maisha yao kwa kuwapa njia mbadala ya kujipatia kipato na hivyo kuachana na ukataji wa miti hovyo na uvuvi usio endelevu. 

Timu ya wataalamu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) sambamba na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya wakiwa katika usafiri wa kiberenge kulekea eneo liloathirika na mafuriko ya maji na mvua Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro.

Kupitia mradi huo, Halmashauri ya Nyasa imefanikiwa kupanda miti takriban 3,500 rafiki kwa vyanzo vya maji, kupunguza ukataji holela wa miti kwa kutoa elimu ya matumizi ya majiko banifu yanayotumia kuni chache.

Muonekano wa juu kwa baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ya mvua katika Halmashauri ya Mlimba.

Mradi huo unatekelezwa katika halmashauri za wilaya zingine za Mbinga (Ruvuma), Kyela (Mbeya), Ludewa na Makete (Njombe) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi