Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mbarawa Azindua Safari Za Ndege za KIA - Dubai.
Dec 15, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_24990" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirika la Ndege la FlyDubai mara baada Waziri huyo kuzindua safari za shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro leo. Katikati ni Makamu wa Rais Uendeshaji Biashara wa Shirika hilo, Sudhir Sreedharan.[/caption]

Serikali imesema itahakikisha inatoa ushirikiano kwa Shirika la Ndege la Dubai (Fly Dubai) ili kuhakikisha inafanya kazi zake vizuri za utoaji wa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.

Akizungumza leo mkoani Kilimanjaro katika uzinduzi wa safari za ndege kutoka Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) kuelekea nchini Dubai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa uzinduzi wa safari hizo utakuza sekta ya utalii na biashara mkoani humo na nchi kwa ujumla.

"Naamini kupitia uzinduzi huu uchumi wetu utakua kwani wafanyabiashara na watalii kutoka nchi mbalimbali wataweza kuongezeka zaidi sababu wamesogezewa huduma za usafiri wa ndege za kimataifa katika viwanja vya ndege vikubwa nchini", amesema Waziri Prof. Mbarawa.

[caption id="attachment_24991" align="aligncenter" width="750"] Wageni waalikwa wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la FlyDubai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro leo.[/caption] [caption id="attachment_24992" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira (kulia), Makamu wa Rais Uendeshaji Biashara wa Shirika la Ndege la FlyDubai, Sudhir Sreedharan (wa pili kushoto) wakikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa safari za Ndege za Shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro leo.[/caption] [caption id="attachment_24993" align="aligncenter" width="750"] Makamu wa Rais Uendeshaji Biashara wa Shirika la Ndege la FlyDubai, Sudhir Sreedharan, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, madaraja mbali mbali yaliyoko kwenye ndege ya Shirika hilo, wakati wa uzinduzi rasmi wa safari zake katika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Mkoani Kilimanjaro leo.[/caption] [caption id="attachment_24994" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Eng, Christopher Mukoma, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika jengo la abiria katika uwanja huo, Mkoani Kilimanjaro leo. Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano[/caption]

Aidha, Profesa Mbarawa ameuhakikishia uongozi wa shirika hilo la ndege kuwa hawatojutia uamuzi wao wa kuamua kusogeza huduma zao za usafiri katika uwanja huo kwani wafanyabiashara wengi na wananchi kutoka sehemu mbalimbali wamekuwa wakitumia uwanja huo.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirika la ndege la Dubai, Sudhir Sreedharan, amesema kuwa kutokana na umuhimu na ubora wa uwanja huo wameamua kusogeza huduma zao kutokana na kuamini kuwa wageni wengi wa kimataifa wamekuwa wakitumia uwanja huo kwenda sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii mkoani humo na mikoa ya jirani ya Arusha na Manyara.

"Kuna mambo mengi yametuvutia kuanzisha safari zetu katika uwanja huu, tunaamini hata soko letu la biashara litafanikiwa kwa kuongeza huduma hapa", amefafanua Makamu wa Rais.

Shirika la ndege la Dubai, sasa litatoa huduma za usafiri wa anga katika viwanja vya ndege vitatu kikiwemo kilichozinduliwa leo cha KIA na vile viwanja viwili vya ndege vya Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa ndege wa Zanzibar vilivyokuwa awali.

Imetolewa na

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi